Kampuni ya Toshiba imeamua kutoa FlashDisks zenye KeyPad ambazo zitakuwezesha kuweka Password katika Flash yako ili kuweza kufunga na kufungua Data zako pindi unapozihitaji.
Hata hivyo flash hiyo endapo utaipoteza na mtu akaiokota akijaribu kuingiza tarakimu kadhaa mara 10 ili kujaribu kubashiri passwords itafuta Data zote mara moja. Hii husaidia haswa kiusalama Data zako zisiweze kuvujishwa na watu.
Pamoja na hayo FashDisks izo zitakua zikipatikana kwa ukubwa kuanzia 4GB, 8GB, 16GB, na 32GB  na bei kuanzia $95 USD hadi $200 USD


SlashGear



Post a Comment

 
Top