Lockheed Martin SR-71 (Blackbird)
Lockheed Martin SR-71(Blackbird)
Lockheed Martin YF-12
Ndege aina ya Lockheed SR-71 maarufu kama
"Blackbird" ndiyo ndege
inayo kwenda kwa spidi zaidi duniani. Ndege hiyo ambayo ilitengenezwa na
kampuni ya kutengeneza ndege hususani za kijeshi ya nchini Marekani ijulikanayo
kama Lockheed Martin ilianza kutengeneza ndege hiyo walipoandaa project yao
ijulikanayo kama Black Project.
Ndege hiyo ilishapewa majina ya
utani kama “Blackbird na Habu. Tangu mwaka 1976 ndege hiyo imeshikilia rekodi
ya kuwa ndege inayo kimbia zaidi duniani ikiipiku rekodi ya ndege iliyokuwa
ikijilikana kama YF-12. Blackbird ina kwenda kwa spidi ya Kilomita 3,529.6 km/h kwa saa, sawa na Maili
2,193.2 mph kwa saa.
Hata hivyo, Ndege hiyo ya
Blackbird SR-71 ilianza kutumiwa na jeshi la Marekani U.S. Air Force mnamo mwaka 1964 hadi 1998. Kampuni
hiyo ilitengeneza ndege za aina hiyo zipatazo 32 na ndege 12 zilipata ajali
lakini ajali hizo hazikuwa za kushambuliwa na maadui.
Post a Comment