Antonov An-225 Mriya ikiwa imebeba Buran Spaceplane (Space Shuttle)

Ndege aina ya “Antonov An-225 Mriya” ndiyo ndege kubwa na nzito kuliko zote duniani na imetengezwa na Antonov Bureau Designs ya  Umoja wa nchi za Kirusi pamoja na Ukraine miaka ya 1980 na kumalizika mwaka 1988. Ndege hiyo itumiayo engine za Turbo injini zipatazo Sita na zime jigawanya katika kila bawa moja Turbo injini tatu.
Ndege hiyo ya Antonov An-225 Mriya ni ndege inayo tumika kusafirishia mizigo mikubwa katika nchi mbalimbali duniani hata hivyo ilitengenezwa kwanza kwa ajili ya kubebea ndege ijulikanayo kama Buran SpacePlane na ina uwezo wa kubeba uzito wa 250,000 Kilogramu kwa mizigo ya ndani na kubeba 200,000 Kilogramu kwa juu kama (Energia Rocket’s boosters na Buran Spaceplane)  na pia ndege hiyo ilianza kuruka kwa mara ya kwanza tarehe 21 Disemba 1988.
Hata hivyo ndege ya Antonov An-225 Mriya ina Kruu (crew) ya marubani wapatao sita , ina urefu wa futi 275 na inchi 7, Bawa lake lina futi 290, ikiwa tupu bila mzigo ina uzito upatao  285,000 kilogramu, uzito wake mwisho wakati wa kutaka kupaa ni 640,000 kilogramu na pia spidi yake ni Kilomita 850 kwa saa.
Pamoja na hayo, ndege ya pili aina hiyo hiyo ya Antonov An-225 Mriya ilianza kutengenezwa kidogo kidogo mnamo mwishoni mwa miaka ya 1980 ambayo ilkua ni maalumu kwa kusafirishia mizigo na hiyo ni baada ya kuanguka kwa Umoja wa nchi za Kirusi mwaka 1991 na kuamua kusitisha matumizi ya Antonov An-225 kubeba Buran spaceplane.
Kufikia mwaka 2000 ndege ya pili ya Antonov An-225 mafanikio ya kukamilika kwake yalianza kuonekana na wakaamua ifikapo Septemba 2006 iwe imesha kamilika lakini ikachelewa kukamika na kuanzia Agosti 2009 ikawa bado haia kamilika na kuamua kuifutilia mbali mpango huo wa kutengeneza ndege hiyo. Ilipofika Mei 2011 mkuu wa mradi huo wa kutengeneza ndege hiyo ali ripoti na kusema kuwa kuna hitajika kiasi cha Dola za kimarekani Million 300 sawa na Shillingi za Kitanzania Billioni 48 na kama wakiwezeshwa kupata kiasi hiko cha fedha basi mpango wa kukamilisha ndege hiyo itachukua miaka mitatu.

Antonov An-225 Mriya imejipatia umaarufu mkubwa kwa kua ndege nzito na kubwa kuliko zote duniani na kuvunja rekodi ya kuwa ndege kubwa duniani ikifuatiwa na ndege zingine kama Airbus A380, Boeing 747-400ER, Antonov An-124 Ruslan na Lockheed C-5 Galaxy.

Post a Comment

 
Top